ufafanuzi_banner_2.jpg

Karibuni wote kwenye tovuti ya Kanisa la Biblia Publishers

Hongera kwa nia yako ya kusoma Neno la Mungu. Tunategemea tunaweza kukusaidia kwa njia mbalimbali ili ulielewe na kulitangaza Neno la Bwana na kueleza ujumbe wa Yesu Kristo kwa watu walio karibu na walio mbali. Chunguza tovuti hii vizuri ili ujipatie vitabu vinavyofaa kwa maisha na huduma yako. Vitabu vyetu vinapatikana katika maduka mbalimbali ya Kikristo katika nchi ya Tanzania. 

MPYA

Ufafanuzi Hai wa Biblia (Believer‘s Bible Commentary) ni kitabu kinachotoa maelezo ya kila mstari wa Biblia kwa upana na kwa kina sana. Katika nyaraka zake Mtume Paulo, anahimiza maisha ya kushirikiana vema katika familia, katika Kanisa na katika jamii. Pia analieleza Kanisa limwone Yesu Kristo ili lijiandae kwa kurudi kwake.