Ukifanya utafiti kuhusu nyenzo zilizotumiwa ili kumsaidia mtu kuokoka au kuanza kutafakari kuhusu Mungu, utagundua kuwa watu wengi mara ya kwanza waliguswa na maandiko kwa kusoma kipeperushi walichokiokota au kupewa na mtu.
Karatasi zinazobeba ujumbe wa Mungu zinaweza kugawiwa kwa njia nyingi. Je, njia hiyo ya kumpatia mtu usiyemfahamu au unayemfahamu karatasi ili akisome na kukitafakari bado ni njia inayofaa siku hizi? Je, watu wanapokea na kusoma machapisho? Au tutafute njia nyingine za kugawa maneno ya Injili, kwa mfano njia ya mitandao ya jamii, kama vile facebook au whatsapp?
Uinjilisti wa Maandiko ni huduma ya Kusambaza Injili kwa njia ya maandishi, vielelezo na mtandaoni kwa lengo la kusaidia watu wamjue Mungu, wapate kuokoka na kukua Kiroho.
Hapa nataka kutoa ushauri kuhusu huduma za kuwafikia watu kwa njia ya Maandiko au vielelezo. Faida kubwa ni kwamba ujumbe unawafikia watu wengi.
Maandalizi ya muda mrefu
Kuwaombea watu wanaohitaji kufikiwa ili kila mtu apate ujumbe ule unaomgusa na kumbadilisha. Omba uongozi wa Roho Mtakatifu ili ujue unaende wapi, utampa nani ujumbe wa Mungu na utasema nini naye ukimkadhi karatasi.
Maandalizi ya muda mfupi
Upange mahali pa kwenda na kusambaza maandiko ukiwa unamfuata mteja pale alipo, k.m. kazini, ofisini, hospitalini, kanisani, sokoni na sehemu nyingine.
Uchague traksi unazozifahamu ili uweze kutoa vipeperushi vinavyofaa katika mazingira husika. Uwe makini ukitafuta vipeperushi. Chagua vile unavyoweza kugawa. Zingatia lugha wanayotumia.
Weka vipeperushi katika mfuko wa plastiki angavu ili uweze kulinda karatasi isikunjike na ionekane haraka vilivyopo. Inafaa kusoma traksi zote kabla ya matembezi.Kila traksi ina ujumbe maalum kwa mtu katika hali fulani aliyonayo. Tumia Biblia ya karatasi unaposhuhudia.
Faida ya kugawa traksi (vipeperushi)
Usiposumbua watu una uhuru wa kuongea na watu wote na kuwauliza kama wanapenda kupokea karatasi yenye ujumbe muhimu. Wakiwa tayari unaweza kuwaeleza Injili na kuwaombea. Vilevile unaweza kuwasaidia kupata ushauri wa maisha na unaweza kusikiliza shida zao katika ndoa au familia au nguvu za giza. Ni furaha kubwa ukiweza kumwonesha mtu mmoja njia ya wokovu na kumwongoza sala ya toba.
Usigawe katika umati mkubwa bali umpe kila mtu baada ya kuongea naye na kumwelewa. Umweleze umuhimu wa kusoma Neno la Mungu na kuokoka kutoka kwenye dhambi.
Kugawa traksi (vipeperushi) kwa njia ya kijitali
Kwa njia ya e-mail na whatsapp unaweza kugawa maudhui (maneno) ya traksi ukimtumia rafiki yako .pdf na kumwuliza ameelewa nini. Hata masomo ya Emmaus shule ya Biblia yanaweza kusomeka kwa njia ya Emmaus-App. Emmaus App inamruhusu mtumiaji kusoma masomo yote yaliyojazwa na kusoma Biblia ya NENO.
Kazi ya msambazaji wa maandiko ni nini?
Kuwatia MOYO na kuwapa watu TUMAINI kwa maisha yao.
Kuwatangazia UKWELI wa Mungu kuhusu hukumu ya Mungu na uzima wa milele.
Kuwaongoza il wakakate shauri na kuingia kwenye NJIA YA WOKOVU.
Kwajumla huduma hiiinaleta mabadiliko kwa jamiiili wapate tumainikwa maishayao.
Ushauri kwa msambazaji wa maandiko
Uiombee kazi hiyo na uwe na watu wanaokuombea. Uwaarifu kuhusu mambo ya kuombea na majibu ya maombihayo.
Ni vizuri kukumbuka na kushirikisha ushuhuda. Hata watoaji wa traksi wanapenda kusikia itikio la wasomaji na changamoto za mgawaji.
Nguvu ya Maandiko
Mwandishi wa Vitabu Samuel Zwemer (Mmisionari katika Mashariki ya Kati 1890-1929) aliandika hivi:
“Machapisho ni mmisionari anayefika kote kwa bei ndogo. Yanapenya mipaka ya nchi zilizofungwa (kwa Injili) na yanawafikia watu wa matabaka yote. Kitabu hakichoki kusomeka, hakihitaji kurudi nyumbani, kina Maisha marefu kuliko wamisionari na wachungaji waliokiandika au kukiuza. Kinapenya mioyo, fikra na dhamiri za watu. Matokeo yake yanaweza kupatikana kote, hata kama kitabu kimesahaulika kinaweza kuendelea kufanya kazi kikishikwa tena baada ya miaka mingi.”
Hapa unaweza kuangalia traksi 9 za kupakua na traksi 5 za kimaandishi.
Comments